## PR22/265 — Bodi Tendaji ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Yaidhinisha Mpango wa Mkopo kwa Tanzania

## Source details

**Canonical URL:** [PR22/265 — Bodi Tendaji ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Yaidhinisha Mpango wa Mkopo kwa Tanzania](https://www.imf.org/-/media/files/news/press-release/2022/pr22265-swa-tanzania-pr.pdf)

## Other formats

- [Markdown version](/-/media/files/news/press-release/2022/pr22265-swa-tanzania-pr.pdf.md)
- [Structured JSON version](/-/media/files/news/press-release/2022/pr22265-swa-tanzania-pr.pdf.json)

---

### Uidhinishaji wa Mkopo na Mipango ya Fedha
- Bodi Tendaji ya IMF imeidhinisha mpango wa mkopo kwa Tanzania wenye thamani ya SDR milioni 795.58 (sawa na dola za kimarekani milioni 1,046.4), ambapo dola milioni 151.7 zitatolewa mara moja.
- Mpango wa mkopo ni wa muda wa miezi 40 chini ya mpango wa ukopeshaji wa ECF (Extended Credit Facility).
- Makubaliano chini ya mpango wa ECF yanafuatia mkopo wa dharura wa dola milioni 561.5 za Kimarekani (sawa na asilimia 100 ya sehemu ya Tanzania IMF) zilizotolewa kwa Tanzania mwaka 2021.
- Makubaliano haya yanatarajiwa kuchochea upatikanaji zaidi wa misaada ya kifedha kutoka kwa nchi nyingine na mashirika mengine ya kimataifa.

### Malengo ya Mpango na Msingi wa Sera
- Lengo la mpango wa miezi 40:
  - kusaidia kufufua uchumi na kukabiliana na athari za vita ya Urusi na Ukraine,
  - kusaidia kuhifadhi uthabiti wa uchumi jumla,
  - kusaidia mageuzi ya kimfumo ili kuendelea kuwa na ukuaji endelevu wa uchumi wenye kuhusisha watu wote, kutokana na vipaumbele vya serikali.
- Mpango unatokana na vipaumbele vilivyoko kwenye Mpango wa Maendeleo wa serikali wa Miaka Mitano.
- Msaada wa kifedha kutoka IMF unatarajiwa kusaidia kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi na kuchochea misaada zaidi ya kifedha kutoka kwa washirika wa maendeleo.

### Vipaumbele vya Mageuzi na Matumizi ya Fedha
- Mageuzi yatazingatia:
  - kuimarisha mfumo wa matumizi ya serikali ili kupata fedha zinazohitajika kwa ajili ya matumizi ya huduma za kijamii na uwekezaji wa sekta ya umma wenye tija zaidi,
  - kuanzisha tena na kuendeleza mageuzi ya kimfumo,
  - kuimarisha na kuendeleza huduma za fedha.
- Walihimiza kuongeza mapato ya serikali, kusimamia vizuri matumizi, na kudhibiti hasara za kifedha za serikali zinazoweza kusababishwa na mashirika ya umma, miradi ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi, na serikali za mitaa.

### Tathmini ya Wakurugenzi wa IMF (Kaimu Mwenyekiti)
- Wakurugenzi walipongeza serikali kwa namna ilivyokabiliana na hali ya uchumi kutokana na janga la UVIKO-19 na sera ilizotekeleza ili kupunguza athari kutokana na vita nchini Ukraine.
- Wakurugenzi walitambua kwamba changamoto kwenye maendeleo na mageuzi pamoja na vipingamizi kutoka nje (UVIKO-19 na vita nchini Ukraine) vinahatarisha mafanikio makubwa ya uchumi.
- Wakurugenzi waliunga mkono maombi ya serikali kupewa mkopo wa ECF ili kukidhi mahitaji muhimu.
- Wakurugenzi walisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi za wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19.
- Walifurahishwa na dhamira ya serikali ya kusawazisha matumizi kwa kupeleka fedha zaidi kwenye huduma za kijamii na kuboresha ufanisi na usimamizi wake.
- Wakurugenzi walisisitiza umuhimu wa kuwa na mkakati wa kujenga uwezo unaohusisha watu wote ili kurahisisha juhudi za kufikia mageuzi makubwa.

### Mapendekezo ya Sera na Hatua za Kudhibiti Hatari
- Kuhakikisha hatua za kukabiliana na kupanda kwa bei za mafuta na vyakula zinazingatia umakini na zinakuwa za kipindi kifupi.
- Kutozidisha mikopo yenye masharti ya kibiashara ili kuhakikisha deni la taifa linaendelea kuwa himilivu.
- Kuendeleza uwazi kwenye masuala ya mapato na matumizi ya serikali na uwajibikaji.
- Kupunguza ujazo wa fedha pale itakapohitajika, huku ikiruhusu thamani ya shilingi ya Tanzania iendane na nguvu ya soko ili kupunguza athari zinazoweza kutokea.
- Kutahitaji mkakati mzuri wa mawasiliano kwa ajili ya sera ya fedha ya Benki Kuu ya Tanzania.

### Sekta ya Fedha, Udhibiti na Mtazamo wa Mazingira
- Kuboresha kanuni za fedha, usimamizi na utekelezaji wa mapendekezo ya tathmini ya sekta ya fedha ya mwaka 2018 (Financial Sector Assessment Program 2018) ni muhimu katika kukabiliana na mapungufu kwenye sekta ya fedha.
- Hatua zaidi zinahitajika katika kuunganisha mfumo wa kuthibiti fedha haramu (AML/CFT) na muongozo wa kikosi kazi cha kimataifa kijulikanacho kama “The Financial Action Task Force (FATF)”.
- Wakurugenzi walihimiza serikali kutekeleza mpango wa mageuzi ili kuimarisha uwekezaji wa sekta binafsi na ukuaji wa uchumi, kwa pamoja na:
  - kuboresha uwezo wa nguvu kazi,
  - kuongeza matumizi kwenye miundombinu,
  - kuondoa mwanya uliopo katika kufikia usawa wa kijinsia.
- Ni muhimu kuboresha takwimu za Pato la Taifa.
- Walisisitiza haja ya kuendelea na juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, kwa kuanza na matokeo ya tathmini ijayo ya usimamizi wa uwekezaji wa umma unaozingatia mabadiliko ya tabia ya nchi, yaani Climate-Public Investment Management Assessment (C-PIMA).

*Source: PR22/265 — IMF press release (Swahili).*

---


_Source: https://www.imf.org/-/media/files/news/press-release/2022/pr22265-swa-tanzania-pr.pdf_
